REMEMBERING SWAHILI WORDS - PART 5

Part 1 | Part 2 | Part 3 |Part 4 | Part 5 | Part 6 |

 

 to Zanzibar Photos Page

 

Swahili Lyrics

Mwiba wa kujitoma

01.

Nani alokusukuma, kisima kile
Siwape waja kusema, wata kelele
Ni mwiba wa kujitoma, hambiwi pole
Ni mwiba wa kujitoma, hambiwi pole (chorus line)

02

Uliyodhaniya siyo, ya muafaka
Usiulaumu moyo, kwa kuteseka
Kwa pupa na zako mbio, umeanguka
Ni mwiba wa kujitoma, hambiwi pole

03.

Wa kukuweza hapana, kiumbe wewe
Umepoteza dhamana, tuwa utuwe
Ungaruka mbawa huna, ewe kunewe
Ni mwiba wa kujitoma, hambiwi pole

04.

Ni hakika watu utu, huutambui
Wapenda mtu kwa kitu, damu si mai
Sindano kiwa na kutu, huishonei
Ni mwiba wa kujitoma, hambiwi pole

05.

Leo umejulikana, kijungu meko
Na hiyo yako khiyana, ndiyo umbo yako
Ulichokiata jana, leo si chako
Ni mwiba wa kujitoma, hambiwi pole

Maneno Tisiya

01.

Nina maneno tisiya
Ukipenda niridhiya
Na ukiiza nambiya

06.

Tano wata mshangao
Usiche watunenao
Watu hawatundi yao

02.

Mwenda kiri sinikere
Nipa siniteze shere
Kwakima ama kwabure

07.

Sita wakufanya domo
Yaliyo ndani ya momo
Sotaa una tomomo

03.

Pili kheri niridhiya
Sikunena neno piya
kuwa litakutukiya

08.

Sabaa wata kelele
Yao ni ya teletele
Asohili una lile

04.

Na la tatu nimekiri
Ukiwa nawadhahiri
mimi nifanya wasiri

09.

Na la nane ndoo zako
Silali kwa hamu yako
Uwe wangu niwe wako

05.

Nne sina budi nawe
Simtaki mginewe
N'ondesha nami nituwe

10.

La tisiya nishawiri
Sinichelee khatari
Bora ni wewe kukiri

 

 

Part 1 | Part 2 | Part 3 |Part 4 | Part 5 | Part 6 |

 

 to Zanzibar Photos Page

 

 

Quick Names Index

 

 

Copyright © Fazals 1999 - All Rights Reserved